Saturday, January 14, 2012

Newsflash: Hon. Regia Mtema, a special seat Member of Parliament from Kilombero representing CHADEMA political party has died in car accident around Ruvu bridge in Coast region!!


Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinasikitika kutangaza kifo cha mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Taifa, Mheshimiwa Regia Mtema (pichani) ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum na Waziri Kivuli wa Kazi na Ajira. 

Mheshimiwa Regia Mtema amefariki leo tarehe 14 Januari 2011 kwa ajali ya gari katika eneo la Ruvu darajani.

Katika uhai wake marehemu Regia Mtema amefanya kazi mbalimbali za kisiasa na kijamii katika taifa. Marehemu Regia Mtema amezaliwa tarehe 21 mwezi Aprili mwaka 1980 na kusoma shule za sekondari kidato cha kwanza mpaka cha sita katika shule ya sekondari ya Forodhani na Shule ya Wasichana ya Sekondari ya Machame. Marehemu Regia Mtema alipata shahada yake ya kwanza (Bsc Home Economics and Human Nutrition) katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine.

Mara baada ya kuhitimu masomo yake marehemu Regia Mtema alifanya kazi katika taasisi mbalimbali kabla ya kujiunga na CHADEMA na kuteuliwa kuwa Afisa Mwandamizi katika Kurugenzi ya Vijana ya CHADEMA na baadaye kuteuliwa kuwa Afisa Mwandamizi katika Kurugenzi ya Mafunzo ya CHADEMA nafasi ambayo aliishikilia hadi mwaka 2010 alipoteuliwa kuwa mbunge wa viti maalum

CHADEMA inatoa pole kwa familia ya marehemu Regia Mtema, wanachama wote na wananchi wa Mkoa wa Morogoro hususani wa Jimbo la Kilombero kutokana na msiba huu wa ghafla katika wakati ambapo mchango wake ukihitajika kwa chama na kwa taifa.

Imetolewa na,

John Mnyika(Mb)
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
Chadema

No comments:

Post a Comment