Friday, February 3, 2012

TABASAMU penye dhiki...kulikoni picha ya kiofisi kuumbwa na TABASAMU...?!

Picha moja huwakilisha maneno zaidi ya elfu moja. Huweza kueleza hisia ya mtu na hata tabia kwa ujumla. Zipo aina mbalimbali za picha, na hupigwa kwa malengo tofauti. Mojawapo ni picha inayopigwa kwa lengo la matumizi ya kiofisi, mfano kitambulisho, Pasi ya Kusafiri na zinazofanana na hizo. Kwa leo nitaizungumzia "Portrait" ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete.

Kawaida, Rais aliye madarakani anapaswa kuwa na picha katika ofisi mbalimbali za umma na hata zile binafsi ikiwa ishara ya kumtambua kama kiongozi halali wa Nchi. Picha hii ni moja ya picha zinazotumika katika mchakato huo na ni rahisi kuikuta katika ofisi mbalimbali za Serikali na Binafsi. Tatizo langu na picha hii ni "TABASAMU" la Mhe. Rais. Nilitegemea picha hii ingeundwa na Sura isiyoonyesha hisia yoyote (Neutral expression) kwa kuwa zipo sehemu haiwezi kulandana na tafsiri yake. Kwa mfano, Hospitalini, polisi na sehemu zingine zisizohitaji kumuona Rais akitabasamu.

No comments:

Post a Comment