Tuesday, December 27, 2011

Kwanini Daraja lililopo karibu na kambi ya JKT Mikocheni halikuyumba wakati wa mafuriko..?!

Moja ya athari kubwa zilizoletwa na mvua kubwa iliyonyesha katika ukanda wa Pwani ikiwemo Jiji la Dar es salaam ni uharibifu wa miundo mbinu ya Barabara hasa sehemu zilizounganisha barabara na madaraja. Maeneo ya Kawe kuelekea Mbezi Beach na Tegeta yalijikuta yakikosa huduma muhimu ya usafiri baada ya Barabara zake mbili kufungwa kutokana na kubomoka kwa madaraja yanaunganisha maeneo hayo (kawe Bondeni na Rain Bow - njia ya chini). Hata hivyo Daraja la muda lililojengwa na Jeshi la Kujenga Taifa eneo la Mikocheni halikuathiriwa kabisa jambo lilinifanya nichunguze kulikoni.

Ugunduzi: Sababu moja kubwa niliyogundua ni muundo mzuri wa kupitisha maji (mitaro). Ukiangalia picha hapo juu utagundua kuwa madaraja mengi yaliyoathiriwa ama kubomolewa hayana njia nzuri za kupitisha maji kuelekea Baharini au pengine kusahaulika kwa njia za mito (njia nyingi zilikuwa zimegeuzwa dampo) na kufanya maji kutafuta njia mbadala. Tishio la mvua nyingine kubwa limetangazwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa na changamoto iko pale pale. Tujiandae kwa Mafuriko wandugu.

No comments:

Post a Comment