Thursday, December 29, 2011

Kwa wasanii wetu mnaolalamika kuibiwa kazi zenu, someni hii!!

Filmu iliyopata kushika katika tasnia filamu za Action "Fast five" imetajwa na mtandao wa Torrent Freak kuwa ni miongoni mwa filamu zilizoongoza kwa kuibwa kupitia njia mtandao kwa mwaka 2011. Mtandao huo unaonyesha kuwa filamu hiyo ilinyonywa kutoka kwenye mtandao wake na watumiaji milioni 9.2, ikifuatiwa na The Hangover II kwa watumiaji milioni 8.8 na filamu zingine ikiwemo Thor ( 8.3mil)), thriller Source Code ( 7.9mil) na I Am Number Four (7.6mil).

Mitandao mbalimbali imekuwa ikitumiwa kupitisha filamu kinyume cha sheria (Pirates) ikiwa ni kampeni za wanaharakati katika nchi zilizoendelea kusaidia wasio na uwezo kupata filamu hizo bila kulipia. Mitandao hiyo imewezesha watumiaji wa mtandao kunyonya filamu mbalimbali bila makubaliano na wamiliki au wasanii husika na hivyo kushusha mauzo. Nchini Tanzania wizi wa kazi za filamu hutumiwa zaidi kwa njia ya kunyonya ama kutoa nakala za CD/DVD kinyemela pamoja na watumiaji kuazimana. Hata hivyo Wataalamu katika masuala ya mitandao na utayarishaji wa filamu wanashauri mtindo mpya wa kutayarishaji movie kwa kutumia teknolojia ya 3D ambayo si rahisi kunyonywa kwenye mitandao na huhitaji kifaa maalum cha miwani kutazama filamu za aina hiyo.

No comments:

Post a Comment