Thursday, December 22, 2011

Social Media outstripped mainstreaming media in Tanzania

Katika kile tunachoweza kukieleza kuwa dunia ya utandawazi tumeshuhudia "social Media" zikivipiku kwa kiwango cha juu Mainstreaming media au vyombo vya habari katika kutoa taarifa ya majanga mbalimbali ikiwemo hili la sasa (mafuriko jijini Dar) na lile la kuzama kwa Boti ya MV islanders kule visiwa vya Nungwi. Hadi kufika sasa kundi kubwa la watu zikiwemo media zenyewe wamekuwa wakitegemea taarifa kutoka kwenye mitandao mbalimbali huku Facebook na twitter zikiongoza kwa karibu mjadala wa janga hilo. Hii ni adhari kwa waandishi na wadau wa sekta ya habari na wawe tayari kwa mabadiliko makubwa zaidi. Hadi kufikia sasa Tanzinia inakadiria kuwa na watumia zaidi ya laki nne (400,000) katika mtandao wa facebook na nusu yao wakiwa na akaunti katika twitter.

No comments:

Post a Comment