Monday, January 23, 2012

Kwanini watu wengi hupenda kwenda kusoma nchi za Magharibi?


Elimu ni ufunguo wa maisha, kauli hii iliwahi kuwa maarufu miaka ya 70 hadi 90 (sina uhakika kama bado inaaminiwa tena) na iliwahi kutumika kama chachu ya kuhamasisha vuguvugu la elimu barani Africa. Kadri siku zinavyozidi kusonga mbele ndivyo gharama za elimu zimeendelea kuongezeka mara dufu. Pamoja na ongezeko hilo bado watu wengi wamekuwa wakikimbilia vyuo vya nje ikiwemo ulaya na Marekani ingawa takwimu zinaonyesha kuwa gharama ni kubwa kwa zaidi ya mara kumi ya zile wanakotoka. Kwa mfano, gharama za kusoma mwaka mmoja ngazi ya shahada nchini Marekani inafika Pesa za kitanzania milioni 30, huku shahada hiyo hiyo hugharimu kiasi cha milioni 2 hadi 5 za kitanzania.

Uchunguzi unaonyesha kuwa kuna tofauti kubwa ya ubora wa elimu inayotolewa kati ya nchi zilizoendelea na zile za dunia ya tatu. Kwa mfano ni rahisi sana kwa mwanafunzi wa uandishi wa Tanzania kumaliza shahada yake bila kujua chumba cha habari au kushika kifaa husika, wakati mwanafunzi wa fani hiyo hiyo katika nchi zilizoendelea akamaliza akiwa ameshaajiriwa katika chombo cha habari au kuanzisha cha kwake. Hii imetajwa kuwa sababu kubwa inayochelewesha maendeleo barani Afrika kutokana na ukweli kuwa wataalam wengi wanakosa ubunifu na uwezo baada ya kujifunza nadharia katika miaka yao yote ya mafunzo.  

No comments:

Post a Comment