Saturday, February 11, 2012

Dawa za ARVs zathibitika kuzuia maambukizi ya Virus Vya Ukimwi!!

Hii ni habari njema kwa watu wanaoishi na VVU na jamii kwa ujumla:

Matokeo ya tafiti mbalimbali zilizofanyika Afrika na sehemu zingine duniani zimethibitisha kuwa kuna uwezekano wa zaidi ya asilimia 96 kwa mtu anaeishi na Virus vya Ukimwi kutowaambukiza wapenzi wao endapo watatutumia Dawa za kupunguza makali ya VVU kwa usahihi. Tafiti hizo ambazo baadhi zililazimika kusitishwa kabla ya muda wake uliopangwa baada ya matokeo ya awali kuonyesha mafanikio makubwa.

Kwa mujibu wa kampuni ya Kimarekani ya Utengenezaji wa Dawa za Kupunguza makali ya VVU - (tenofovir na emtricitabine), Gilead Science, imekili kusitisha tafiti zake kabla muda uliotegemewa kumalizika baada ya matokeo ya awali kuonyesha mafanikio makubwa katika nchi za Kenya na Uganda.

Kampuni hiyo iliendesha tafiti hizo kwa kuangalia matumizi ya sasa ya ARV ikiwemo huduma ya Post Exposure Prophylaxis (PEP) ambayo hutumiwa kuzuia maambukizi ya VVU kwa wahudumu wa afya wakati wa utoaji wa kuwahudumia wagonjwa, ambpo mhusika hupewa dozi hiyo ndani ya saa 72 baada ya kupata VVU, na ile ya Mama mjamzito dhidi ya mtoto wake wakati wa kujifungua (PMTCT).

Jumla ya wapenzi 4758 walihusishwa katika utafiti wa PrEP (Matumizi ya ARVs kwa watu wasio na VVU - Kinga). Katika utafiti huu, wapenzi wawili (mmoja mwenye VVU na mwingine asiye na VVU) walihusishwa kwa kutumia dawa aina ya tenofovir na emtricitabine (TDF/FTC). Utafiti huu ulionyesha kuwa matumizi ya dawa hizi kwa kila siku unaweza kupunguza uwezekano wa kuambukizana kwa aslimia 95. Hakukuwa na dalili ya athari zozote kwa dawa zote wakati wa matumizi hayo. Pia utafiti kama huo ulifanywa chini ya Mtandao wa Utafiti dhidi ya VVU (HPTN), ambao uliwahusisha wapenzi (discordant couples 1750) kwa kipindi cha miezi 78 katika nchi za Afrika, Asia na Marekani. Utafiti huo nao ulikoma baada ya mwaka mmoja kutokana na matokeo kuonyesha mafanikio makubwa

Tafiti hizi pia zimeibua hoja mpya ya muda unaofaa kwa watu wenye VVU kuanzishia "dozi ya ARVs" baada ya nchi mbalimbali kutofautiana eneo hilo. Hadi sasa nchi nyingi zinazoendelea ikiwemo Tanzania, zimekuwa zikitumia Muongozo wa WHO ambao unapendekeza watu wanaoishi na VVU waanzishiwe Dozi hizo wanapofikisha CD4 kuanzia 350 kuja chini. Hata hivyo nchi za Marekani na Ulaya zimekataa kutumia muongozo huo na badala yake huwaanzishia watu wao mara wanapogundulika kuambukizwa au wanapofikisha CD4 kuanzia 500 na kuendelea. Hii inasemekana kuwa inaweza kutoa majibu ya kuwepo kwa tofauti kubwa ya watu wanaoishi na VVU, Maambukizi mapya na hata vifo vingi katika nchi maskini hasa Kusini ya Jangwa la Sahara, Barani Afrika na zile zilizoendelea za Ulaya na Marekani.

PAMOJA NA YOTE, HADI SASA HAKUNA UTAFITI ULIOFANYWA JUU YA FAIDA NA HASARA YA KUWAANZISHA DAWA HIZO MAPEMA.



Imeandaliwa na;
Dotto Athumani
Producer/Report
Graduate School of Journalism
UC Berkeley.
California.


contact: mnyadi@berkeley.edu, +1 (510) 666 7345

No comments:

Post a Comment