“Nawaambia kwa amri hii Kafulila amekula sumu, ilikuwa halmashauri ikutane na kurejea tena uamuzi wetu dhidi yake na wenzake, lakini kwa amri hii ya Mahakama haiwezi kukutana na sasa tumefungwa mikono, na tunaendelea na uamuzi wetu wa kumsimamisha hatutachukua uamuzi mwingine hadi kesi ya msingi iishe,” Haya ni maneno ya mwanasheria na Mkuu wa Idara ya Katiba na Sheria, NCCR-Mageuzi, Dk Sengondo Mvungi alipokuwa akitolea ufafanuzi juu ya sakata la kufukuzwa uanachama Mbunge Kijana, David Kafulila na wenzie.
David Kafulila ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kusini, hivi karibuni alivuliwa uanachama na chama hicho na kupoteza sifa ya kuendelea na kiti chake cha Ubunge kwa mujibu ya katiba (Diwani, Mbunge au Rais atakoma nafasi hiyo endapo atavuliwa uanachama wa chama anachokiwalisha!!!). Hata hivyo kafulila alichukua hatua ya kupinga uamuzi huo Mahakamani na hatimaye kurejeshewa nafasi yake hadi kesi ya msingi itapofikia mwisho.
No comments:
Post a Comment